News

Attention: open in a new window. PDFPrint

Udahili wa Wanafunzi wa Shahada ya Uzamili(M.A) Katika Kiswahili


Maombi yanakaribishwa toka kwa wenye sifa za kujiunga na Progarmu ya Masomo ya Shahada ya Uzamili katika Kiswahili, inayotarajiwa kuanza mwezi Oktoba, 2009. Waombaji wa kike wenye sifa wanahimizwa watume maombi kwa wingi.

Malengo ya Programu:

• Kuandaa wataalamu watakaofundisha Kiswahili katika vyuo vya elimu ya juu; • Kuandaa wataalamu wa Kiswahili watakaofanya kazi katika vyombo vya habari, tasnia ya uchapishaji, idara za serikali, mashirika ya kimataifa pamoja na maeneo mengine yanayohitaji wataalamu wa aina hiyo; • Kuandaa wanafunzi watakaojiunga na mafunzo ya uzamivu (PhD) katika Isimu na Fasihi ya Kiswahili; • Kuandaa magwiji wa uandishi wa kubuni, tafsiri, ukalimani na utungaji wa Kamusi.

Walengwa

Wale wote wenye raghba katika Isimu, Fasihi na Utamaduni wa Kiswahili na ambao wanahitimu shahada zao za kwanza katika nyanja za Isimu na/au Fasihi

Muda wa Mafunzo

Kama ilivyo kwa kozi nyingine za Uzamili zinazotolewa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, muda wa mafunzo kwa kozi hii utakuwa miezi 18. Hata hivyo muda huo utaweza kuongezwa kwa kuzingatia matatizo ya kiafya na kijamii yanayokubalika kichuo.

Muundo wa Programu

Programu hii inahusu vipengele vikuu viwili vya taaluma ya Kiswahili, ambavyo ni Isimu na Fasihi ya Kiswahili.Mwanafunzi atakayedahiliwa katika programu hii atahudhuria masomo katika semista mbili kwa mwaka mmoja wa masomo na atawajibika kuchukua jumla ya kozi 12 (zinazokamilisha jumla ya vizio 36). Wanafunzi ambao watabobea zaidi katika Isimu watalazimika kuchukua pia kozi mbili za fasihi ya Kiswahili na kwa wale ambao watabobea zaidi katika Fasihi, itawabidi kuchukua pia kozi mbili za isimu. Katika semista moja kila mwanafunzi atalazimika kukamilisha kozi zenye jumla ya vizio 18.

Mwanafunzi ambaye atakuwa amefaulu majaribio pamoja na mitihani yake atalazimika kufanya utafiti na kuandika tasnifu itakayotoa mchango halisi wa maarifa na kudhihirisha kuwa mhusika amebobea vya kutosha katika fani ya taaluma aliyochukua.

Lugha ya Mafunzo

Lugha itakayotumika katika mafunzo ya Programu hii itakuwa Kiswahili.

Sifa za kudahiliwa

Shahada ya kwanza ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au ya Chuo Kingine kilichodhibitishwa na Tume ya Vyuo Vikuu vya Tanzania (TUT). Sifa ya chini kabisa ya kudahiliwa kwa mwombaji ni ufaulu katika shahada ya kwanza wa kiwango cha daraja la pili cha wastani wa GPA ya 2.8. Aidha ufaulu katika masomo ya isimu na fasihi yaliyochukuliwa katika shahada kwanza wa wastani wa GPA 3.0

Uandikishwaji

Uandikishwaji kwa wale watakaopata udahili utafanywa tu kwa wale watakaodhihirisha kuwa wana uwezo wa kulipa ada husika za masomo, ambazo zitalipwa ama moja kwa moja na mwanafunzi mwenyewe au na MDHAMINI wake. Kwa vyovyote vile, ushahidi wa kimaandishi utahitajika kuthibitisha kwamba mhusika anao uwezo huo.

Ada

Kwa waombaji ambao ni Watanzania: Shilingi 1,577,500/= kwa mwaka wa kwanza, na kwa miaka inayofuata:shilingi 1,302,500/= kwa miezi 6 au shilingi 1,752,500/= kwa miezi 12. Kwa waombaji ambao sio Watanzania: Dola za Kimarekani $ 2,446 kwa mwaka wa kwanza na kwa miaka inayofuata: $2622 kwa miezi 6 au $ 3,374 kwa miezi 12. Kiasi hicho hakitajumuisha gharama za mwanafunzi za moja kwa moja kama zilivyobainishwa katika tovuti ifuatayo: www.udsm.ac.tz au http://postgraduate.udsm.ac.tz

Namna ya Uombaji

1. Wale wote wenye sifa na ambao wangependa kuomba kudahiliwa wachukue fomu katika Taasisi ya Taaluma za Kiswahili, Jengo la Kiswahili, Chumba namba 208.

2. Fomu za kuombea udahili zinapatikana pia katika tovuti ya Taasisi ya Taaluma za Kiswahili:www.iks.ac.tz

3. Fomu ya maombi italipiwa ada ya maombi ambayo haitarejeshwa ya jumla ya Shilingi elfu ishirini, kwa waombaji ambao ni Watanzania au Dola za Kimarekani $ 20 kwa waombaji wasio Watanzania. Ada hiyo ilipwe kwa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili: Jina la Akaunti IKS PUBLICATION A/C, Namba ya akaunti 040-1030-00213, NBC Bank, Mlimani Branch. Swift Code NLC BTZ TX, SLB 35181, DAR ES SALAAM.

4. Fomu ya maombi iambatishwe na nakala zilizothibitishwa za vyeti halisi

5. Watu binafsi, mashirika pamoja na vyombo binafsi vinahimizwa kuwadhamini waombaji wenye sifa kupitia Mfuko wa Shaaban Robert wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili. Kwa taarifa zaidi kuhusu Mfuko huu wasiliana na Mkurugenzi.

6. Fomu za uombaji zilizojazwa vizuri ziwe zimerejeshwa kupitia anuani iliyotajwa hapa chini IFIKAPO TAREHE 30 SEPTEMBA 2009.

Anuani

Mkurugenzi,
Taasisi ya taaluma za Kiswahili
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
S.L.P. 35110
DAR ES SALAAM

e-mail: This e-mail address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it